Тёмный

Salama Na MR BLUE SE6 EP69 KHERI PART 2 SendTip MPESA LIPA NO 5578460 

YahStoneTown
Подписаться 395 тыс.
Просмотров 77 тыс.
50% 1

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
Kheri Sameer aka Mr Blue aka Lil Sama aka Bayser ni mdogo wangu, mdogo wangu kabisa na uzuri nakumbuka kabisa mara ya kwanza kuonana nae na mpaka alivyokua amevaa. Jezi ya Denver Nuggets, jeans ya light blue na sneakers nyeupeeehh na chain ya Silver, kwenye maskio alikua na hereni za kung’ara zile ambazo zilikua si za kitoboa skio, zilikua zina smaku na nazijua zaidi kwasababu Marehemu cousin brother wangu alikua nazo maana nyumbani ilikua hairuhusiwi kutoboa maskio enzi hizo. Alikua msafi, ana swagg ya kuongea na hata jinsi alivyokua anajibeba. Alikua wa moto sana unaweza kusema hivyo, au niseme hivyo. Kila ‘mtoto’ na kijana alitamani kuwa kama yeye kwa kila kitu, muonekano mpaka hit songs kwenye radio na TV.
Blue alikua na mtu ambaye anamsimamia na huyo hakua mwengine bali G Lover, meneja na Dj ambaye alikua anasimamia kazi zake yeye pamoja na wasanii wengine kama Ally Kiba, Ally Com na Abby Skills kwa kuwataja kwa uchache na wasanii wake hao wote walikua wa moooto sana. Ngoma kali, video mbaya, show nyingi na kwa ‘mhindi’ wanauza sana. Na kuanzia hapo kwa mhindi na kuuza sana ndo ambapo kuliweza kuwapoteza wengi kwasababu wengi walikua wadogo sana na pesa ilikua nyingi. Fitna na utovu wa nidhamu wa kupindukia ulianzia hapo. Wakati naandika hii nilimuwaza Ally Kiba na jinsi ambavyo ameweza ku maintain class flani toka siku ya kwanza tunamskia na mpaka leo regardless ya mengi ambayo yametokea hapo katikati, HAKUWAHI KUPOTEA. Kwa hilo naamini anastahili HESHIMA na recognition ya hali ya juu pengine kuliko tunayompa maana dah, mambo yalikua mengi sana enzi hizo.
Kuna usemi kwamba wakati ni mwalimu mzuri sana na kwa uelewa wangu hakuna ambaye anaweza kuelezea experience kama ilivyo elezewa kwenye usemi huo. Wakati ndo ambao unatufunza na kutuonyesha vitu na watu wengi, ambao tulikua tukiwaamini na wengine kuto kuwaamini, kuwapenda na wengine kuto wapenda, kudhani unajua na ki ukweli hujui, kudhania umezama kwenye dimbwi na mapenzi na huyo alo nae ndo wako wa milele na kumbe si hivyo na hayo yote unayaelewa within kipindi fulani, miaka inavyokwenda ndo na wewe unaelewa na kujifunza mambo kwa uwezo na uelewa wako. Moment za ‘anha’ na ‘wow’ huwa nyingi sana. Wakati ni MWALIMU na majuto huwa ni mjukuu, nadhani utakua umenielewa.
Mr Blue alikua na dunia kwenye miguu yake, ilikua yeye tu aseme anatakaje na anataka ielekee wapi na hivyo ndo ingekua ila haikua hivyo ndo jambo la kusikitisha lakini bahati kubwa ambayo mwenzetu alikua nayo au yuko nayo ni kwamba hayo yote yalitokea mapema sana, wakati yuko mdogo sana kwenye dunia ambayo wengi walikua wakimuangalia na kumpenda sana. Yeye baada ya kuona mapenzi na shangwe hilo basi akadata na akaanza kuwa mgumu kufanya nae kazi, akawa na marafiki tele ambao hakua anawajua kabla hajawa Lil Sama na baadae Mr Blue. Akawa hasikii la muadhini wala mnadi sala. Akajiingiza kwenye uvutaji wa bangi isokua na staha, akaondoka nyumbani na kwenda kuishi kwenye ma ghetto na wana wasokua na ramani. Akawa ana party Jumatatu mpaka Jumatatu. Studio haonekani, kwenye interview hatokei na wale watangazaji ambao walikua wanapiga mgoma zake kwenye Radio akawa hata salaam hawapi. Producer na meneja nao wakagombana nae kwasababu sitofahamu ya pesa kwa mhindi ilishika hatamu.
Mwanzo nilisema Blue ana Kheri sana kama jina lake kwasababu hayo yote yalitokea wakati mdogo sana, dunia ilimfunza nae akafundishika, wakati dunia hiyo ikiwa inamfunza alikua mwanafunzi mzuri sana kwasababu darasa alilolipata wakati kakata ringi ndo ambalo limefanya awe BORA na ajitambue LEO HII.
Kwenye meza yetu ya kigae na kiti chakavu Blue ananielezea hustle zote ambazo alishawahi kuzipitia wakati anakua na huku akiwa anajitafuta na kwa uelewa wangu itasaidia wengi ambao wanaaza au wataanza kuzishika pesa mapema au hata ambao watapata mafanikio huko mbeleni watajua jinsi ya ‘kujibeba’ kutokana na maongezi yetu haya.
Tafadhali enjoy.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahStoneTownSubs
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪RU-vid Link bit.ly/RU-vidSalamaNa
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz

Развлечения

Опубликовано:

 

28 май 2023

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 212   
@pillyjuma3095
@pillyjuma3095 Год назад
Anaongea Kwa kituo .anampa nafas host, anajibu alichoulizwa... The best interview ever..
@Basagamp4
@Basagamp4 Год назад
Hakika....Mahojiano yanaleta raha
@javanwatson6675
@javanwatson6675 Год назад
raha ya kuangalia Interview za Blue ni moja; una uhakika kua hawezi kudanganya
@rehemaothman2475
@rehemaothman2475 Год назад
❤❤❤❤umegonga ndipo
@shabanigenya4708
@shabanigenya4708 Год назад
@@rehemaothman2475mwamba saaana huyo
@mwanaiditwaha8341
@mwanaiditwaha8341 Год назад
Umeona eeeh nampenda je tangu utoto
@awadhally1052
@awadhally1052 Год назад
😄kwel
@maitharobert6833
@maitharobert6833 Год назад
💯
@richardcastromzena5136
@richardcastromzena5136 Год назад
1:52 truth 2:40 🔥 8:00 Mungu 16:53 Hatujaumbwa wabaya 17:30 Mungu ni mwema 17:58 Wema 21:22 Elimu
@evergreenmushi2171
@evergreenmushi2171 Год назад
The "dadangu" part kwa kila anapojibu 🙌
@mtanojuma3809
@mtanojuma3809 Год назад
ukimsikiliza vizuri bayser kuna madini fulani anayo history yake ya maisha inafundixha san
@abdulsalimsalim7533
@abdulsalimsalim7533 Год назад
Yah! kabisa yan kuna vipande lzm urudishe nyuma upate madini
@gtunewaves2867
@gtunewaves2867 Год назад
This is not just an interview but this is THERAPY
@barbarasara4033
@barbarasara4033 Год назад
Asante ❤❤❤❤
@alijafar9098
@alijafar9098 Год назад
Sure🙏🇰🇪
@bstechtz7414
@bstechtz7414 Год назад
Mr Blue Byser 🎉🎉 umelisha ubongo wangu leo, Msaani wangu pendwa all the time
@PatrickGianna-lg5zz
@PatrickGianna-lg5zz Год назад
Am blessed,,,,am hoping to stop alcoholic life,,,,forbidden my family lkn hop God blesses me
@nassorntandu4513
@nassorntandu4513 Год назад
Umepiga nyundo kubwa sana Mr Blue, hasa kwa vijana wa kisasa ambao wamejitupa kwenye maovu na wanaona huo ni ujanja! Kwa historia Yako na ushuhuda wako umewafunza wengi Sana, wakubadilika watabadilika!
@amossichinga7231
@amossichinga7231 Год назад
Nimeipenda sana hii interview ametoa mafunzo mengi sana ya maisha, nawakubali sana
@martinfrancis9808
@martinfrancis9808 Год назад
DADA SALAMA YANI LEO UMENIKOSHA NAMKUBALI SANA MR BLUE... NIMEFURAHI SASA MTAFUTE ...DIAMOND PLATNUM
@queenmariposa799
@queenmariposa799 Год назад
Best interview ever.... Byser upo so humbled hadi Dada Salama kafurahi
@misanyamisanya7499
@misanyamisanya7499 Год назад
Safi Da salama kwa kumrekebishaa Blue sio vijumba jumba ni NYUMBA watu hawana ataa iko kibanda kwaiyo asikae kinyongeee😀😀😀😀
@mickthomas-lh1fs
@mickthomas-lh1fs Год назад
Aisee salama naweza kusema hii ni moja ya yastone town nzuri sana sana kuliko ndani ya miezi hii iliyopita kuwahi kutokea.
@Dawah99
@Dawah99 3 месяца назад
One of the interviews of all time. Dude is so real and humble maa shaa Allah. Pia napenda how Salama adjusts ndani ya interview. Kudos 👌🏾
@hamadymwanja3564
@hamadymwanja3564 Год назад
Kweli blodar blue mie nimependa point ambayo hata mie naiamini kwenye maisha yangu ya kuwa hakuna kinachoshindikana chini ya juwa kila kitu Ni Maamuzi tuu
@cdeleo9336
@cdeleo9336 Год назад
Una akili sana i hope vijana wengi wataangalia hii interview na kujifunza kitu
@zuwenazuwena7764
@zuwenazuwena7764 Год назад
What a humble guy ❤ inever expect Mr blue ataongea hivi yoooooo 😮❤❤ olive it ❤
@adamkapolo8817
@adamkapolo8817 Год назад
This man is very realistic
@innocentmushi1550
@innocentmushi1550 Год назад
Blue anamheshimu sana Salama, anavyomuita "dada yangu" unaona kabisa heshima anayomuonyesha.
@wardahwamras6976
@wardahwamras6976 Год назад
Nnapo zidi kumpenda blue Mister...Nikumtaja mwenyezi MUNGU 🤲 kwa kila jambo..endelea kumtukuza Allah
@kazkaz1943
@kazkaz1943 Год назад
Best interview ever 🎉
@juliusamani4002
@juliusamani4002 Год назад
Salama & Blue aisee nyie ni watu wema sana...Mungu azidi kuwabariki
@esterdoriye8377
@esterdoriye8377 Год назад
Nimejifunza vingi sana hii interview ☺ 🤗 😊 💓 🙂
@raymondmuga7542
@raymondmuga7542 Год назад
Nice interview, it's very organic
@murarayvan5732
@murarayvan5732 Год назад
Apa Rwanda tunamupenda na tunamukubali sana Mr blue
@turukimedia
@turukimedia Год назад
SALAMA SIKU HIZI WAGENI WAKO HAWAPATI MSOSI NAONA MR BLUE AJALETEWA MSOSI HAPO...
@MohamedAbuu-ty6jy
@MohamedAbuu-ty6jy Год назад
Please 🙏🙏. Dada salama tuletee Saigon dada 🙏🙏🙏
@hajirashid2049
@hajirashid2049 Год назад
❤❤ yah ukiongea na mtu asiyekuwa na kona kona unaelewa zaidi na tumemuelewa sana jah bless you all.
@tinomasangia5511
@tinomasangia5511 Год назад
The best interview so far
@abrahamamu5456
@abrahamamu5456 Год назад
Superb Interview!... Host yupo real, Mgeni ndio kabisa!
@jamilaathumani5481
@jamilaathumani5481 Год назад
Hongera salama jabir kwakujua kuhoji ,,ukihojiwa na salama lazima utapike yooote,, hongera salama Kwa hilo
@evasonlushaka767
@evasonlushaka767 Год назад
Msanii wangu wa kipindi hicho. Mungu azidi kukubariki niliumia Sana wakati wa Maputo yako. But am happy you are ok and the gone go
@jamilaathumani5481
@jamilaathumani5481 Год назад
Umeongea point blue,,vipaji vinapotea kwer Kwasababu ya hela
@mugoliciroyi5088
@mugoliciroyi5088 Год назад
Iyi interview ime ni tunza moyo ❤Mungu awabariki
@sofiasophia9018
@sofiasophia9018 Год назад
Sikuhizi hakuna chakula salama naona maji ila mwamba anasemaga ukweli 2❤❤
@salimkombo9767
@salimkombo9767 Год назад
The Best interview ever!!!!!!!
@newswireKenya
@newswireKenya Год назад
ALL TIME FAVOURITE TANZANIA HIT MAKER, MR BLUE LONG LIVE SIR
@justinejackson1731
@justinejackson1731 5 месяцев назад
Dah! Thanks Blue na Salama..hii ni zaid ya interview kiukweli..hili ni darasa huru juu ya maisha na mapito yake🙏🙏
@GeofreyNasson-vu9lf
@GeofreyNasson-vu9lf Год назад
Akili mingi bysa🙌🙌
@farajagideon8170
@farajagideon8170 Год назад
Mr Blue una hekima ya ki Mungu, hongera sana kaka!❤❤
@nomar3708
@nomar3708 Год назад
Nampenda sana kijana huyu. Yupo very real. Unaangalia interview in mafunzo na hapo hapo you have a smile on your face. Mola akubariki kaka yangu
@lekorollenewton5601
@lekorollenewton5601 10 месяцев назад
Mr blue my all time favourite...the best interview this year.
@shaabanramadhan6770
@shaabanramadhan6770 Год назад
Kunamafunzo nimepata marafiki wengi ni wanafki napia tuchague marafiki jambo la mwisho tusikate tamaa kwenye maisha
@innocentmushi1550
@innocentmushi1550 Год назад
👍
@Joliegal834
@Joliegal834 Год назад
Ili swali la unga aliulizwa na salama kweny mkasi miaka 10 iliyopta na alijibu jibu hilihili 😊
@hawasaid7151
@hawasaid7151 Год назад
Interview bora sana Big up Mr blue❤❤
@MbogoCharles-ov9xw
@MbogoCharles-ov9xw Год назад
Sister salama upo makni sn kwa swali ety make umemuuliza huyo jamaa vyamsingi sna dada angu ongera sn pia Allah akutangulie kwakila jambolako 🙏🙏🙏🙏
@user-kt7yi9hv3n
@user-kt7yi9hv3n Год назад
Mr Blue one love brother pamoja na sister salama
@oscarmario466
@oscarmario466 Год назад
Huyu jamaa alifanya maombi binafsi ambayo mungu huyasikia moja kwa moja huwa yanaambatana na toba
@paschalmichael7250
@paschalmichael7250 Год назад
Nilichojifunza kwa bayser ni kwamba, tunapokuwa kwenye Maisha ya ujana huwa tunahelemewa sana na starehe hasa na pesa ukiwa unapata lakini pia ukiweza kupata nafasi ya kujifunza kwa watu muhimu ipe nafasi akili yako kuyapokea yale yoote yaliyo mazuri kwasababu yanakujenga watu wanajuwa kuwa unakosea akili yako pia inajuwa ila kichwa ngumu, lakini ugumu wa maisha utakufanya ukubaliane na maneno ya baadhi ya watu kuwa kwa sasa unabidi ubadilikeeee, Its babylon bayser quotes
@mubahurio4710
@mubahurio4710 Год назад
Nakuelewa sana blue in shaa Allah akulipe
@bellarmeeuma1653
@bellarmeeuma1653 Год назад
Next Salama na Stamina,Salama na Bushoke,Salama na Afande Sele.
@peterassenga2428
@peterassenga2428 Год назад
Rapper Wangu Bora wa muda wote
@tembagentil
@tembagentil Год назад
Nawakubali woote wa wili❤
@kazkaz1943
@kazkaz1943 Год назад
Yaan hapa najiuliza baada y hii interview kip niangalie cha kunijenga zaid sio upuuz au nizime data ibak hii kichwan week
@mgallason...5686
@mgallason...5686 Год назад
Big brain
@dengahmediatz1230
@dengahmediatz1230 Год назад
Blue ni yanga bana🖤💚💛
@mosesmaryz3535
@mosesmaryz3535 Год назад
Jamaa yuko real sana I like that
@davidwalalason7630
@davidwalalason7630 Год назад
Byser hizi experience zilete Kwa muziki
@kassimakida1666
@kassimakida1666 Год назад
Narudi ndio my favorite song kutoka kwa huyo mwamba ataree saana
@benjaminsemwenda3152
@benjaminsemwenda3152 Год назад
Role model wangu wa muda wote Babylon Byser Beezy kwenye game
@RomanusSamwel-gd2jq
@RomanusSamwel-gd2jq Год назад
Bonge ya interview Yan unataman isiishe
@tinyobayser3738
@tinyobayser3738 Год назад
That's is Bizzz 🙌🙌 Heshima kubwa sana
@user-sh6rh4ee2h
@user-sh6rh4ee2h Год назад
Tuletee fid q kitambo sana tumemis maneno yake
@mrishojumaamrisho3212
@mrishojumaamrisho3212 Год назад
Thug life❤❤❤,,,!!!..byser be blessed brother
@lilhomies2541
@lilhomies2541 Год назад
my all time favorite artistist.....busy babilon
@abdullysalim5020
@abdullysalim5020 Год назад
Mtu aliepata aka shuka akipanda tena ni mbarikiwa mungu akuongoze
@MohamedAbuu-ty6jy
@MohamedAbuu-ty6jy Год назад
Mr blue mtu poa sn, respect sn kk
@affleckmusic3709
@affleckmusic3709 Год назад
thanks s.jabir naomba next tuletee mr Nay the true Boy
@andrewireri4305
@andrewireri4305 Год назад
What an Amazing Interview,Mr Blue your very mature and inspiring,much love from 🇰🇪
@shabanigenya4708
@shabanigenya4708 Год назад
Umeeendika pouwa saana Salama.
@natashasuleiman962
@natashasuleiman962 Год назад
The best interview bless you all 💯 tunamtakaaaa diamond platnumz
@letsunwrap5954
@letsunwrap5954 Год назад
Best interview! Such growth. Much love
@kingwattanlibz9391
@kingwattanlibz9391 Год назад
Aliyengoja hakuwahi kuja....nimeipenda iyo salama
@bish_daddiyao
@bish_daddiyao Год назад
Inspirer of Bongo flavour nice interview Auntie🙌🏾❤️
@neemamsemwa7180
@neemamsemwa7180 Год назад
Niko hapa kwa hyo "Ndo hivyo dada angu"..Sasa angu imetajwa Hadi Raha Kila anapomuita..nimependa
@georgeburchard4872
@georgeburchard4872 Год назад
Hapo kwenye show jukwaani aisee aaah wee Ni shida! Ni wachache Sana wanoweza kukufikia!
@jaybilaly7469
@jaybilaly7469 Год назад
Hongera salama hakika mahojiano mazuri na tunaenjoy
@didakalaule7840
@didakalaule7840 Год назад
Ahsanteni team nzima interview ni nzr mnooo❤❤❤❤
@khadijakimana8809
@khadijakimana8809 5 месяцев назад
Lovely guy! I was wondering when is he...? Manchallah nice to see you again, Mr Blue, I still have your CD I bought back in 2005 😅
@Love4Ril
@Love4Ril Год назад
Genuineness inafanya kitu chochote kiwe na nuru na uhai ndani yake. Ndio kama mfano wa Mr Blu. Nice one!
@mwanaishahassan8738
@mwanaishahassan8738 Год назад
Perfect ✊✊✊
@allycantara3873
@allycantara3873 Год назад
Wakwanza nipeni like
@drkiti
@drkiti Год назад
Just awesomeness👏
@motoredo314
@motoredo314 Год назад
Wema haozi Mr blue.....mungu aendelee kukuongoza
@yousramutwale2463
@yousramutwale2463 Год назад
Nifurai sana n'a hiii interview
@GoodluckAM
@GoodluckAM Год назад
Blue yupo real sana 👍🏽
@samirmswahili
@samirmswahili Год назад
Salute sana intervista 👌
@paulnames6624
@paulnames6624 Год назад
Tasamu imenibadilisha sana pia wazee walisem nimerogwa siitwi show nikatoa pesa ika hit ,aisee kila kituo naenda chek nyimb nd narud kweny interview
@SamBunse
@SamBunse 17 дней назад
Salama naomba interview yako na stamina
@EliasaHassan
@EliasaHassan Год назад
Hivi mnajua kwann. Amejiita nyani zee
@tinyobayser3738
@tinyobayser3738 Год назад
Always Mchizi Namkubali Sana Bayser ✊🏿✊🏿
@amaloy5915
@amaloy5915 Год назад
Very fantastic Show🔥👍😊, Next we ask🙏 for #FidQ #JayMoe #ChristianBella #Hanscana
@robartifabiani
@robartifabiani Год назад
Fid q mbona yupo huku Mzee tafuta
@noxxete
@noxxete Год назад
Ati mtu ngapi pale Kinondoni?🤣🤣...I like how he is just real. Much respect Mr Blue.
@hezelonono9663
@hezelonono9663 Год назад
I love your interviews...would care to add sub titles for non swahili speakers...good job though
@emmakiwaya4607
@emmakiwaya4607 11 месяцев назад
one of the very best interview, very inspiring! Kuna vijana wengi sana wanaweza kuponywa na hii interview its unfortunate sidhani kama wamepata chance ya kuitazama.
@bausonameeeenmunguninimuwe8900
Nakukubali sana byser
@piscoteddyshow8405
@piscoteddyshow8405 Год назад
I do love this dude
@arafatmiraj9926
@arafatmiraj9926 Год назад
All time favorite Blue
@user-cj3xq4gz3s
@user-cj3xq4gz3s Год назад
Namukubali sana Mr blue kutoka Congo Kinshasa
Далее
Копия iPhone с WildBerries
01:00
Просмотров 368 тыс.
Salama Na Idris Ep 8 | TROOPER Part 1
33:07
Просмотров 309 тыс.
Salama Na JOTI Ep 47 | SIMPLY SPECIAL PART 1
35:15
Просмотров 462 тыс.
This or That 🛍️
0:52
Просмотров 5 млн
ИСПАЧКАЛ
0:30
Просмотров 2,5 млн