Тёмный

Utapenda: Makonda alivyogusa Maisha ya Mtoto huyu, kuanzia Arusha hadi Moi kwenye matibabu 

Gilly Bonny Tv
Подписаться 495 тыс.
Просмотров 154
50% 1

MOI YAANZA KUTOA MATIBABU KWA MTOTO GODSON KWA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA.
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili MOI imeanza kutoa matibabu ya kibingwa kwa Godson Mwaipopo (7) ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa Kambi ya Matibabu ya kibingwa yaliyokuwa yanafanyika Mkoani Arusha.
Mtoto Godson ni miongoni mwa mamia ya watoto na watu wazima waliogundulika kwenye Kambi hiyo ya Matibabu iliyokuwa ikiratibiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ambapo Rais Samia amejitolea kugharamia matibabu yao kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili na hospitali na taasisi za afya za umma.
Joyce Mwasakapwela, mama mzazi wa Godson aliyesafiri kwenda Dar Es salaam kusimamia matibabu ya mwanae akiambatana na Mume wake Bw. Isaac Mwasakapwela kwa gharama za Mkuu wa Mkoa wa Arusha, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa Mkoa wa Arusha na wananchi waliomchangia nauli ya kutoka mkoani Mbeya kuifuata kambi ya matibabu mkoani Arusha, akisema anaamini kuwa mtoto wake atarejea katika hali yake ya kawaida.

Опубликовано:

 

2 июл 2024

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии    
Далее